JIPATIE ELIMU YA UFUGAJI NA UDHIBITI WA MAGONJWA YA MIFUGO YAKO

Je, una swali lolote linalohusu kilimo au mifugo? Tuma swali lako kwanye simu namba 0688099408, utajibiwa na wataalamu wetu mara moja

UFUGAJI WA KUKU


UTANGULIZI
Kuku yupo katika kundi la ndege wanaofugwa na binadmu, katika kundi hili la ndege wa kufugwa wapo pia bata, bata mzinga, bata bukini, njiwa, na kanga. Njiwa, bata na bata mzinga walianza kufugwa zaidi ya miaka 3,000 iliyopita nchini China. Kuku nao yasemekana walianza kufugwa miaka hiyohiyo wakitolewa katika misitu ya ndege ya Kiasia. Baaday ndege wakaanza kufugwa sehemu mabalimbali za bara la Marekani na Ulaya wakiwafuga kwa njia ya kienyeji. Mnamo karne ya 16 kuku waliingia Marekani wakitokea Ulaya na bata mzinga wakaingia Ulaya wakitokea Marekani. Njia za kisasa za uanguaji wa mayai zilianza kutumika miaka ya 1870 lakini si kwa hatua ya kibiashara katika nchi za China na Misiri ya zama hizo. Ufugaji wa ndege kwa njia ya kisasa ulianza kutumika kuanzia karne ya 19 katika bara la Marekani na Ulaya wakilenga katika uboreshaji wa nyama na mayai. Tafiti na mbinu mbalimbali za ujengaji wa nyumba, ulishaji wa ndege, na uzalishaji wa kuku zilizoibuliwa zilipelekea kukua kwa kasi kwa ufugaji wa ndege na hasa kuanzia miaka ya 1930. Laikini ufugaji huu na ulaji wa ndege na mazao yake uliongezeka kwa kiasi kikubwa zaidi wakati wa vita kuu ya pili ya dunia kulipotokea uhaba wa nyama ya ng'ombe na nguruwe. 
Nchini Tanzania haijulikani ni lini ufugaji wa ndege ulianza kufanyika, lakini huenda ulianza mara baada ya kuanza kuwa na makazi kutohamahama na hasa wakati wa utawala wa mkoloni. Kulingana na sensa ya mwaka 1994, idadi ya ndege iliyokuwa inafugwa wakati huo ilikuwa ni 29 685 220 na kati ya hawa kuku wa kienyeji walikuwa 20 163 811 na wa kisasa walikuwa 521 411 (wa nyama-368, 933 na wa mayai-152 478). Ndege wengine wakiwa bata na bata bukini 743 472, bata mzinga 63 447, na kanga 37 942. Idadi hii imeongezeka sana kwa miaka ya karibuni kulingana na watu wengi kuvutiwa na ufugaji wa kuku na ndege wengine kwasababu ya faida zinazopatikana kwenye ufugaji wa ndege. Makadiro ya mwaka 2008 yalionyesha kuwa Tanzania ilikuwa na kuku milioni 36 na kati ya hao asilimia 95 ni kuku wa kienyeji, waliobaki ni wa kisasa.

FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU
Ukimtaja kuku katika maisha ya Mtanzania hakuna asiyemfahamu ama kwa kumuona au kwa kumla na hivyo kufanya kuwa kitu muhimu sana katika maisha ya kila siku. Asilimia kubwa ya Watanzania wanafuga kuku tena kuku wa kienyeji au kwa jina jingine kuku wa kijijini kwa vile asilimia kubwa (80%) ya wafugaji wa kuku wa kienyeji wapo vijijini. Kwa udogo wake, kuku amekuwa ndo mnyama rahisi wa kuchinja kwa kitoweo nyumbani, wajapo ndugu, jamaa na marafiki kutembelea familia. Hivyo kuku hawa wanafugwa kwa malengo makuu mawili; kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya nyumbani na kwa ajili ya kuongeza kipato katika familia. Kuku anafaida zifuatazo; 
1. Kutumika kwa chakula na hivyo kupunguza tatizo la upatikanji wa protini katika familia
2. Kusaidia kuongeza kipato katika jamii na kusaidia kutatua matatizo kwa haraka zaidi maana uuzaji wake ni rahisi.
3. Kuku (jogoo) wamekuwa wakitumika tangu enzi kama saa ya familia wakati wanapotaka kuamka usiku kwa shughuli mbalimbali
Kuku ni mkombozi wa watu wenye kipato cha chini na watu wengi wanapenda kufuga kuku kwa sababu zifuatazo;
1. Watu wengi hasa mijini wanapenda kula nyama ya kuku na mayai hasa kuku wa kienyeji
2. Uwekezaji wa ufugaji wa kuku ni mdogo na hivyo kufanya watu wengei waweze kufuga kuku
3. Upatikanaji wa chakula cha kuku ni rahisi
4. Kuku wanahitaji muda mfupi sana kukua na hivyo faida yake inaonekana mapema
5. Urahisi wa upatikanaji wa dawa na chanjo
5. Gharama za matunzo ni ndogo na hasa kuku wa kienyeji

KUANZA KUFUGA KUKU
Ufugaji wa kuku chinin Tanzania upo wa aina kuu mbili, ufugaji wa kuku wa kienyeji na ufugaji wa kuku wa kisasa. Na kama tulivyokwisha kuona hapo juu ufugaji wa kuku wa kienyeji ndiyo wenye watu wengi zaidi na hii ni kutokana na ufugaji huo kuwa rahisi na usio na gharama kubwa. 
Kabla ya kuanza ufugaji wa kuku (aina yeyote ile) kuna mambo ya msingi ya kuzingatia ili ufugaji wako uwe endelevu na wenye kukuletea manufaa makubwa na faaida zilizoainishwa hapo juu. Mtu yeyote anayetaka kufuga kuku lazima awe na dhamira ya dhati ya kutaka kufuga kuku maana kwa njia hii atawafuatilia kwa ukaribu na kuwapa mahitaji ya msingi ili waweze kuzaa matunda yaliyotarajiwa. Anapaswa akae chini na kupanga kabla ya kuanza ufugaji wake, sehemu hii ya awali ya muhimu na haipaswi kurukwa na tena anayetaka kufuga kuku  ni vema akapata ushauri toka kwa wataalamu wa mifugo au wafugaji wengine wenye uzoefu. Anatakiwa ajue ni aina gani ya ufugaji anataka kufanya (wa kuku wa kienyeji au wa kisasa), kuku wa nyama au wa mayai. Yote haya yatategemea na mahitaji ya eneo alipo pamoja na mambo manne ya msingi ya mtaji, shamba/eneo la kufugia, usimamizi na masoko.

KUKU WA KIENYEJI

Endelea kusoma zaidi HAPA namba 1
Sambaza Google Plus
Post a Comment

Kuwa mwanachama

Jumla ya watembeleaji

Samaki

Google+ Followers