Thierry Henry ametangaza kustaafu kucheza kandanda baada ya miaka 20


THIERRY HENRY ATUNDIKA NJUMU
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry ametangaza kustaafu kucheza kandanda baada ya miaka 20. Henry, aliyeshinda Kombe la Dunia mwaka 1998, na ambaye amepachika mabao mengi zaidi kwa klabu ya Arsenal, aliondoka klabu ya New York Red Bulls mwezi huu. Kulikuwa na tetesi kuwa huenda angekwenda kuchezea timu nyingine. 

"Imekuwa ni safari ya kusisimua," amesema Henry, 37. Thierry Henry sasa anajiunga na kituo cha TV cha Sky Sports kama mchambuzi wa soka. Mfaransa huyo, ambaye pia aliwahi kuichezea Monaco, Juventus na Barcelona, alipachika mabao 175 katika ligi kuu ya England na ni wa nne katika wafungaji bora.

 Henry alishinda makombe mawili ya Ligi Kuu ya England, makombe matatu ya FA akiwa na Arsenal aliyoichezea kati ya 1999 hadi 2007.
Aliongeza Kombe la Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Barcelona mwaka 2009 na alirejea Arsenal kwa mkopo, wakati akiichezea Red Bulls mwaka 2012.

Comments

Popular posts from this blog

Alcohol, Aging, and Curing Cancer